Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/01 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 21/01 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 20/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Syria: Watu kumi na mmoja wauawa katika mashambulizi ya anga ya Israel (Shirika lisilo la kiserikali)
 • ELN yakiri kuhusika katika shambulio dhidi ya chuo cha polisi Bogota (taarifa)
Afrika

Watoto zaidi ya Milioni 4 kupewa chanjo dhidi ya surua nchini Somalia

media Kampeni ya chanjo ya suria nchini Somalia WHO

Somalia imezindua kampeni ya nchi nzima ya kuwapa chanjo Mamilioni ya watoto ili kuepuka ugonjwa wa surua.

Shirika la afya duniani WHO inasema watoto zaidi ya Milioni 4.7 kati ya umri wa miezi sita na miaka 10, wamelengwa kupata chanjo hiyo.

Watoto wengine Milioni 1.1 wanalengwa kupata chanjo hiyo katika eneo la Somaliland.

Tayari jimbo la Puntland limeshamaliza kutoa chanjo hiyo iliyotolewa mwezi Januari na watoto 933,000 kupewa chanjo hiyo.

Hatua hii ya WHO imekuja baada ya watoto 2,800 kukumbwa na suria katika majimbo ya Bay, Banadir na Mudug.

Idadi hii imeshuka ikilinganishwa na maambuzi ya 23,000 mwaka 2017 hasa dhidi ya watoto chini ya miaka 10 lakini ikafanikiwa kuwapa chanjo watoto zaidi ya 600,000.

Chanjo hiyo itatolewa katika vituo vyote vya afya nchini humo.

 

 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana