Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MAUAJI-JESHI

Jeshi la Ethiopia lachunguza kuuawa kwa raia katika mpaka na Kenya

Jeshi la Ethiopia limeanzisha uchunguzi kubaini namna raia 9  walivyouawa na wengine 12 kujeruhiwa baada ya kushambuliwa kimakosa katika eneo la Moyale katika mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

Wanajeshi wa Ethiopia wakikimbizana na wapiganaji wa Oromo katika miaka ya hivi karibuni
Wanajeshi wa Ethiopia wakikimbizana na wapiganaji wa Oromo katika miaka ya hivi karibuni wikimedia.org
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema wanajeshi kadhaa wamesimishwa kazi, baada ya kuwauwa raia hao wakati wa makabiliano na waasi.

Jeshi la Ethiopia kwa muda mrefu sasa, limekuwa likipambana na waasi wanaojiita Oromo Liberation Front (OLF) ambao serikali ya Addis Ababa inasema ni magaidi na wanatishia usalama wa nchi hiyo.

Ethiopia imekuwa ikikabiliwa na changamoto za kiusalama tangu mwaka 2016, baada ya maandamano kutoka majimbo ya Oromia na Amhara.

Wakaazi wa majimbo hayo mawili, yanaishtumu serikali ya Ethiopia kwa kuwatenga kimaendeleo.

Hali hiyo imesababisha kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn, huku hali ya hatari ikitangazwa kwa muda wa miezi sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.