Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-UPINZANI

Wanasiasa wa upinzani wamuunga mkono Katumbi kuelekea Uchaguzi Mkuu

Wanasiasa wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekutana nchini Afrika Kusini na kukubaliana kumuunga mkono Gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi Chapwe kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Moise Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC anayeishi nje ya nchi
Moise Katumbi mwanasiasa wa upinzani nchini DRC anayeishi nje ya nchi © AFP / PHIL MOORE
Matangazo ya kibiashara

Katumbi ambaye alikimbia nchi hiyo, alikutana na wanasiasa wenzake kwa siku tatu jijini Johannesrburg kuweka mikakati ya namna ya kuchukua uongozi wa nchi hiyo kutoka kwa rais Joseph Kabila.

Mwanasiasa huyo amewaambia wanasiasa zaidi ya 100 kuwa, kuungana kwao ni kukataa udikteta na kuweka mipango ya kujega nchini mpya baada ya Uchaguzi wa Desemba.

Pamoja na hilo, ameshtumu Jumuiya ya Kimataifa kwa kumvumilia rais Kabila ambaye amechelewesha Uchaguzi huo ili kuendelea kuongoza.

Aidha, ametilia shaka uwezo wa Tume ya Uchaguzi CENI kuandaa Uchaguzi utakaokuwa huru na haki na kukubaliwa na kila mmoja.

Kumekuwa na maandamano ya mara kwa mara nchini DRC yanayopangwa na Kanisa Katoliki kumshiniza rais Kabila kujiuzulu lakini kutangaza kuwa hatawania urais kwa nguvu.

Rais Kabila hajasema lolote kuhusu hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.