Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kanisa Katoliki na wanaharakati wandaa mgomo kupinga mauaji ya waandamanaji

media Mambo yalivyokuwa jijini Kinshasa wakati wa maandamano yaliyopita REUTERS/Kenny Katombe TPX IMAGES OF THE DAY

Mgomo wa siku nzima unafanyika nchini Jamhuri ya Kidmekrasia ya Congo, kulaani matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya waandamanaji wanaomtaka rais Joseph Kabila kujiuzulu kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Mgomo huu umeratibiwa na Kanisa Katoliki na muungano wa Mashirika ya kiraia nchini humo ambayo yamekuwa yakiandaa maandamano dhidi ya rais Kabila.

Waandamanaji 15 wameuawa na mamia kujeruhiwa katika maandamano ambayo yamekuwa yakifanyika mwaka huu kwa mujibu wa takwimu za Kanisa Katoliki na Umoja wa Mataifa.

Omar Kavota rais wa Shirika la CEPADHO linalopigania uongozi bora na demokrasia, ameiambia RFI Kiswahili kuwa iwapo mgomo huo utaambatana na maandamano, maafisa wa usalama huenda wakatumia tena nguvu kuvunja yavunja na kusababisha maafisa na majeruhi.

Aidha, Kavota amesema huenda maandamano yasisaidie kumwondoa rais Kabila madarakani kama wanaharakati, wanasiasa wa upinzani na Kanisa Katoliki wanavyoshinikiza.

Rais Kabila amekuwa akiongoza nchi hiyo tangu  mwaka 2001 lakini hajatangaza iwapo hatawania tena.

Serikali ya rais Kabila inalishtumu Kanisa Katoliki kwa kuwasaidia wapinzani kutaka kuingia madarakani kwa mlango wa nyuma.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana