Pata taarifa kuu
DRC-MADINI-KABILA

Rais Kabila kutia saini sheria mpya ya madini

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila hivi karibuni anatarajiwa kutia saini sheria mpya ya madini licha ya kupingwa vikali na wawekezaji katika sekta hiyo.

Rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo mpya inaongeza kodi kwa wawekezaji katika sekta hiyo, hatua ambayo huenda ikasababisha wawekezaji kuogopa kuendelea kuwekeza au wengine kuamua kuondoka.

Kinshasa imesema, sheria hiyo iliyopitishwa na bunge mwezi Januari itaanza kufanya kazi hivi karibuni, na yote haya yanakuja baada ya rais Kabila kukutana na wawekezaji siku ya Jumatano.

Waziri wa madini Martin Kabwelulu amesema baada ya mashauriano na wawekezaji hao, rais Kabila amewahakikishia kuwa atashughulikia malalamishi yao baada ya sheria hiyo kutiwa saini.

Wanaharakati nchini DRC wametaka rais Kabila kusaini sheria hiyo haraka iwezekanavyo kwa manufaa ya wananchi wa taifa hilo ambao wameendelea kuishi kwa umasikini licha ya nchi yao kuwa tajiri kwa madini kama Cobalt, dhahabu na madini mengine.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.