Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Viongozi wa ECOWAS walaani mashambulizi ya kigaidi nchini Burkina Faso

media Marais kutoka ukanda wa Sahel barani Afrika , Roch Kaboré (Burkina), Idriss Déby (Tchad), Ibrahim Boubacar Keita (Mali), Mohamed Ould Abdel Aziz (Mauritanie), na Mahamadou Issoufou (Niger) walipokutana na rais wa Ufaransa mwezi Desemba mwaka 2017 REUTERS/Ludovic Marin

Marais wa Togo na Niger wamezuru jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso kusimama na wananchi wa taifa hilo baada ya kundi la kijihadi kushambulia Ubalozi wa Ufaransa na Makao makuu ya jeshi iliyopita.

Mashambulizi hayo yaliyotekelezwa na kundi la GSIM, yalisababisha vifo vya wanajeshi nane na wengine kujeruhiwa.

Rais wa Togo Faure Gnassingbe ambaYe ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS, amesema mataifa hayo yataendelea kushirikiana kwa lengo la kushinda ugaidi Afrika Magharibi.

Naye rais wa Niger Mahamadou Issoufou ambaye ni rais wa nchi za Sahel zinazojumuisha, Burkina Faso, Niger, Mauritania, Chad na Mali, amesema vikosi vya nchi hizi vitaendelea kushirikiana na Ufaransa ili kushinda ugaidi.

Burkina Faso inasema inaendelea kuchunguza namna shambulizi hilo lilivyofanyika, wakati huu rais Roch Marc Christian Kabore akisema itachukua muda mrefu kushinda ugaidi nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana