Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 13/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 12/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Ufaransa: Mmoja wa waandamanaji wanaovalia vizibao vya njao afariki baada ya kugongwa na lori Avignon
 • Raia wa pili wa Canada akamatwa nchini China
 • Uturuki: Watu wanne wapoteza maisha na 43 wajeruhiwa katika ajali ya treni Ankara (gavana)
 • Jerusalemu: Mshambuliaji avamia polisi wawili wa Israel kabla ya kuuawa (polisi)
 • DRC: Ghala la Tume ya Uchaguzi lateketea kwa moto siku kumi kabla ya uchaguzi (mamlaka)
Afrika

Ripoti: Rais Kiir anatumia fedha za mafuta kuendeleza vita

media Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah/File Photo

Ripoti mpya iliyotolewa na wachunguzi wa Global Witness, Shirika la Kimataifa linalochunguza mizozo, matumizi mabaya ya rasilimali na ufisadi, imeonesha namna viongozi wa Sudan Kusini wanavyotumia Mamilioni ya Dola kufadhili vita vinavyoendelea nchini humo.

Imebainika kuwa, fedha hizo zinapatikana kutoka kwenye biashara ya mafuta huku kampuni ya mafuta ikitumiwa kumnufaisha rais Salva Kiir.

Uchunguzi wa Global Witness umebaini kuwa fedha zinazopatikana kutoka kwenye kampuni ya Nile Petroleum au Nilepet, zinatumiwa kukunua silaha zinazotumiwa kupambana na wapinzani wa serikali ya Juba.

Kampuni hiyo inafanya kazi zake kwa siri na mbali na rais Kiir, watu wengine wanaonufaika ni washauri wake wa karibuni.

Wapiganaji wa kikabila nao wananufaika kuhusu biashara hii. Ripoti hii inaeleza kuwa serikali ya Juba iliandikia barua kampuni hiyo kuomba Dola Milioni 1.5 ili kuwalipa wapiganaji wake.

Michael Gibb, kiongozi wa Global Witness amesema walifanikiwa kupata taarifa kuhusu kinachoendelea kupitia mitambo yake ya satelite.

Hata hivyo, kampuni ya Nilepet imekanusa madai hayo na kusema uchunguzi uliofanywa na Global Witness, ni wa uongo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana