Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-MGOMO-HALI YA HATARI

Mgomo nchini Ethiopia kupinga hali ya hatari

Mgomo umeshuhudiwa jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kulalamikia hatua ya serikali kutangaza hali ya hatari nchini humo kwa muda wa miezi sita.

Maandamano jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kupinga hali ya hatari nchini humo.
Maandamano jijini Addis Ababa nchini Ethiopia kupinga hali ya hatari nchini humo. PHOTO | AFP
Matangazo ya kibiashara

Hali ya wasiwasi bado inashuhudiwa katika nchi hiyo bado ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn.

Shughuli za kibiashara zilisitishwa siku ya Jumatatu, huku barabara zikisalia wazi bila ya magari kwa hofu ya makabiliano kati ya waandamaji na polisi.

Sheria ya hali ya hatari inazuia kufanyika kwa migomo na kufungwa kwa barabara katika taifa hilo lenye uchumi mkubwa katika eneo la Afrika Mashariki na Kati.

Raia wa Ethiopia wanalalamikia hatua hii wanayosema inawazuia kufanya shughuli zao kwa uhuru kwa muda wanaotaka.

Hii sio mara ya kwanza kwa Ethiopia kujikuta katika hali kama hii. Mwezi Oktoba mwaka 2016 hadi Agosti mwaka 2017, hali hii ilitangazwa baada ya kuzuka kwa mapigano ya kikabila katika maeneo ya Oromia na Amhara.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.