Pata taarifa kuu
URUSI-MAREKANI-AFRIKA-DIPLOMASIA

Mawaziri wa Mambo ya nje wa Urusi na Marekani wazuru Afrika

Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov anazuru mataifa kadhaa ya bara la Afrika, katika ziara ambayo inaelezwa ni kujaribu kuleta ushawishi wa Urusi kwa bara la Afrika.

Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov
Waziri wa Mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov Vasily MAXIMOV / AFP
Matangazo ya kibiashara

Lavrov alianzia ziara hii siku ya Jumatatu nchini Angola. Ziara hii pia itampeleka Namibia, Msumbiji, Zimbabwe na Ethiopia.

Ziara hii inafanyika wakati huu Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson naye akianza ziara yake barani Afrika.

Anaanzia ziara yake nchini Chad, Djibouti, Ethiopia, Kenya na Nigeria.

Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu wa Marekani barani Afrika tangu kuchaguliwa kwa rais Donald Trump mwaka 2016.

Ziara za wawakilishi wa mataifa haya makubwa duniani, inalenga kuimarisha diplomasia kati ya Moscow na Afrika sawa na Washingtin DC.

Ripoti zinasema kuwa, huenda watakutana jijini Addis Ababa ili kujadiliana kuhusu masuala mbalimbali hasa mzozo wa Syria na mizozo mingine ya bara Afrika.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.