Pata taarifa kuu
DRC-MAANDAMANO-KABILA

Mashirika ya kiraia kuitisha mgomo wa siku moja kulaani mauaji ya waandamanaji

Mashirika ya kiraia yametangaza kufanyika kwa mgomo wa siku nzima siku ya Ijumaa wiki hii, kulaani kuuawa kwa wanaharakati na raia wanaojitokeza kuandamana kushinikiza kujiuzulu kwa rais Joseph Kabila.

Maandamano ya hivi karibuni jijini Kinshasa dhidi ya rais Joseph Kabila
Maandamano ya hivi karibuni jijini Kinshasa dhidi ya rais Joseph Kabila JOHN WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa na Gloria Senga kutoka Shirika linaloshinikiza mabadiliko nchini humo Struggle For Change Movement.

Senga ambaye anaongoza mashirika 14, ameitaka pia Jumuiya ya Kimataifa kusaidia kumwondoa Kabila, ambaye wamemwita dikteta.

Maandamano dhid ya rais Kabila, anayeshinikizwa kujiuzulu yamesabisha watu 17 kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa na Kanisa Katoliki, lakini serikali imekuwa ikikanusha madai ya kuwauwa waandamanaji.

Hadi sasa rais Kabila hajasema iwapo atajiuzulu au hatagombea wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba, kama inavyoshikizwa na waandamanaji.

Maandamano haya yamekuwa yakiongozwa na Kanisa Katoliki nchini humo. Baraza la Maaskofu CENCO ambalo lilisaidia kupatikana kwa mkataba wa kisiasa mwaka 2016 ili kuundwa kwa serikali ya mpito kupitisha Uchaguzi Mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.