Pata taarifa kuu
Guinea-Bissau

Waharakati nchini Guinea-Bissau waunga mkono vikwazo vya ECOWAS

Mamia ya wanaharakati wameandamana jijini Bissau nchini Guinea-Bissau mbele ya makao makuu ya ECOWAS kuunga mkono uamuzi wa Umoja huo wa nchi za Afrika Magharibi, kuwawekea vikwazo watu 19 nchini humo.

Makao makuu ya ECOWAS jijini Abuja Nigeria
Makao makuu ya ECOWAS jijini Abuja Nigeria www.rfi.fr/afrique
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa watu hao mashuhuri waliowekewa vikwazo hivyo ni pamoja na mtoto wa rais Vaz, anayedaiwa kukwamisha utekelezwaji wa mkataba wa kisiasa uliotiwa saini mwaka 2016 jijini Conakry.

Mkataba huu ulifikiwa baada ya mazungumzo kati ya viongozi wa siasa na wadau mbalimbali nchini humo ili kumaliza mzozo wa kisiasa uliozuka nchini humo mwaka 2015.

Mzozo wa kisiasa nchini humo ilikuja baada ya rais Jose Mario Vaz kumfuta aliyekuwa Waziri Mkuu wake Domingos Simoes Pereira.

Msemaji wa wanaharakati hao Domingos Sami amesema wanaishukuru ECOWAS kwa kuchukua uamuzi huo huku wakimlaumu rais Vaz, kwa kukwamisha utekelezwaji wa mkataba huo.

Mkataba huo unataka kuteuliwa kwa Waziri Mkuu atakayekubalika na pande zote za kisiasa ili kuunda serikali ya pamoja, kuelekea Uchaguzi mpya.

Modibo Ibrahim Touré, Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, nchini humo ametaka Jumuiya ya Kimataufa kuisaidai Guinea-Bissau kufanikiwa kutatua changamoto hii ya kisiasa na kutekelezw a kwa mkataba huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.