Pata taarifa kuu
NIGERIA-ITALIA-SHELL-ENI

Kesi dhidi ya kampuni za mafuta Eni na Shell, yahairishwa hadi mwezi Mei

Kesi dhidi ya kampuni za mafuta Eni na Shell, ambazo viongozi wake wanatuhumiwa kwa ufisadi iliyokuwa imepangwa kuanza leo mjini Milan nchini Italia, sasa itaanza tarehe 14 mwezi Mei.

Nembo za kampuni za Shell na Eni
Nembo za kampuni za Shell na Eni www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Jaji aliyekuwa aanze kusikiliza kesi hiyo kutokana na wingi wa kesi katika Mahakama hiyo, kesi hii imeahirishwa.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Eni Claudio Descalzi, na mtangulizi wake Paolo Scaroni na watu wnegine 13 wanatuhumiwa kutoa Dola Bilioni 1.1 ili kupata eneo la kuchimba mafuta ghafi.

Waziri wa zamani wa Mafuta Dan Etete naye pia ameshtakiwa.

Makosa dhidi yao yanadaiwa kuifanya Nigeria kupoteza kiasi kikubwa cha fedha.

Inaelezwa kuwa kampuni hizi zilitoa rushwa ili kupata eneo la kuchimba mafuta yenye uwezo wa kupatikana kwa pipa Bilioni 9 .

Hii ni kesi kubwa ya ufisadi kuwahi kukumba kampuni za mafuta.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.