Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-UGAIDI-UFARANSA

Wanajeshi 12 wauwa baada ya uvamizi wa Ubalozi wa Ufaransa na Makao makuu ya jeshi jijini Ouagadougou

Wanajeshi wanane na wengine 12 walijeruhiwa baada ya watu waliokuwa wamejihami kwa silaha kuvamia ubalozi wa Ufaransa na Makao Makuu ya Jeshi  jijini Ouagadougou nchini Burkina Faso, siku ya Ijumaa.

Jeshi la Burkina Faso likiondoa miili katika makao makuu ya jeshi jijini  Ouagadougou.
Jeshi la Burkina Faso likiondoa miili katika makao makuu ya jeshi jijini Ouagadougou. Issouf Sanogo, AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za kiusalama kutoka kwa serikali ya Ufaransa zimethibitisha mauaji haya na kuongeza kuwa wavamizi wengine wanane waliuawa katika makabiliano hayo makali.

Awali, kulikuwa na ripoti kuwa mashambulizi hayo ambayo pia yalilenga makao makuu ya jeshi la Burkina Faso yalisabisha vifo vya watu 28.

Serikali ya Burkina Faso imesema inachunguza tukio hilo, ili kuwatambua waliotekeleza mashambulizi hayo mabaya hivi karibuni nchini humo.

Hakuna kundi lililojitokeza kudai kuhusika  lakini makundi ya kijihadi yameendelea kuwa tishio kwa serikali ya Burkina Faso na mataifa ya ukanda wa Sahel kama Niger, Chad, Mali na Mauritania.

Waziri wa usalama wa Burkina Faso Clement Sawadogo amesema watu wawili walikamatwa nje ya makao makuu ya jeshi wakati wa uvamizi huo, na kuongeza   kuwa uchunguzi wa awali umeonesha kuwa kulikuwa na gari lililokuwa limejazwa vilipuzi.

Ufaransa ambayo imetuma wanajeshi wake 4,000 katika ukanda wa Sahel, imesema ililengwa katika uvamizi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.