Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Machafuko ya kikabila yaua watu 22 DRC

Machafuko ya kikabila yameua watu 22 mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) siku mbili zilizopita, kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, likinukuu chanzo rasmi.

Askari wa jeshi la DRC wakipiga doria katika kijiji cha Rwangoma baada ya mauaji huko Beni, mji wa mashariki mwa DRC, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Agosti 14, 2016.
Askari wa jeshi la DRC wakipiga doria katika kijiji cha Rwangoma baada ya mauaji huko Beni, mji wa mashariki mwa DRC, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Agosti 14, 2016. Sonia Rolley / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo wa Nyatura, kundi linaloundwa na wanamgambo wengi kutoka jamii ya Wahutu, walishambulia waasi wa kundi la Mai-Mai Yakutumba, wa kikabila ya Nande, katika kijiji cha Kalusi siku ya Jumapili na Bwalanda jana Jumatatu.

Raia kumi na tano ni miongoni mwa waathirika.

Vurugu za kikabila na mashambulizi ya jeshi la serikali dhidi ya waasi vimesababisha vifo vya mamia ya watu katika miezi ya hivi karibuni nchini DRC na maelfu ya watu kulazimika kuyahama makazi yao.

Hayo yanajiri wakatia mabapo hali ya wasiwasi imeendelea kushuhudiwa jijini Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya waasi 4 kuuawa na wengine 7 kukamatwa katika mapigano yaliyotokea katika mji huo kati ya waasi wa Mai Mai na jeshi la DRC (FARDC) mwishoni mwa wiki iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.