Pata taarifa kuu
AFRIKA- UE-G5 SAHEL-USALAMA

Mkutano kuhusu kufadhili kikosi cha G5 Sahel kufanyika Brussels

Mkutano wa wafadhili wa kikosi cha ukanda cha G5 Sahel unafanyika leo Ijumaa, Februari 23 katika majengo ya Tume ya Ulaya mjini Brussels, nchini Ubelgiji.

Askari wa kikosi cha G5 Sahel wakati wa Operation Haw Bi.
Askari wa kikosi cha G5 Sahel wakati wa Operation Haw Bi. RFI/Anthony Fouchard
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa nchi zaidi ya thelathini za Ulaya wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huo pamoja na marais wa tano wa nchi za ukanda wa Sahel.

Washirika wapya kama vile Uturuki, au Afrika Kusini pia watawakilishwa na mawaziri wao wa kigeni. Lengo la mkutano huu ni kutafuta fedha zaidi kwa ajili ya kufadhili mwaka wa kwanza wa operesheni ya kikosi hiki cha pamoja kitakachopambana dhidi ya Boko haramu na makundi mengine ya kigaidi katika ukanda huo.

Mkutano huo utajadili jinsi ya kupata zaidi ya euro milioni 300 ya bajeti iliyotengwa kwa kikosi hiki cha G5 Sahel. Kwa sasa inaonekana kuwa ni vigumu kupatikana kwa kiwango hiki, kwani tayari Umoja wa Ulaya ulikubali kutoa euro milioni 50, huku kikosi hiki kikiwa tayari kimekusanya euro milioni 250. Pamoja na nchi arobaini zitakazowakilishwa katika mkutano huo, waandaaji wa mkutano wana imani kuwa watafikia haraka malengo yao.

Malengo ambayo yanaonekana ni tofauti kwa kila upande. Nchi za ukanda wa Sahel zinabaini kkwamba kikosi cha G5 Sahel kinahitaji euro milioni 423 ili kuanza operesheni yake. Hoja ambayo haiungwi mkono na Ufaransa. "Pamoja na milioni 300, kikosi hiki kina uwezo wa kuendesha operesheni zake za kwanza," Ikulu ya Elysee imebaini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.