Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-UGAIDI

Wanajeshi wawili wa Ufaransa wauawa nchini Mali

Wanajeshi wawili wa Ufaransa wameuawa na mwingine kujeruhiwa baada ya gari walilokuwa wanasafiria nchini Mali, kukanyaga bomu lililotegwa ardhini.

Mwanajeshi wa Ufaransa akilinda usalama mjini Gao nchini Mali
Mwanajeshi wa Ufaransa akilinda usalama mjini Gao nchini Mali FXFreland
Matangazo ya kibiashara

Kuuawa kwa wanajeshi hao kumethibitishwa na Ofisi ya rais Emmanuel Macron.

Taarifa ya Macron hata hivyo haijasema ni eneo lipi nchini Mali, ambako tukio hilo lilitokea.

Hata hivyo, imeelezwa kuwa wanajeshi hao wawili ni wakaazi wa mji wa Valence, Kusini Mashariki mwa nchi hiyo.

Kuuawa kwa wanajeshi hawa, kunafikisha idadi ya wanajeshi wa Ufaransa waliopoteza maisha nchini Mali kufikia 12, tangu kuanza kwa operesheni inayofahamika kama Barkhane mwaka 2012.

Ufaransa ilituma wanajeshi 4,000 nchini Mali baada ya kuombwa kuja kusaidia katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi hasa Kaskazini mwa nchi hiyo tangu mwaka 2013.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.