Pata taarifa kuu
UN-WAHAMIAJI-USALAMA

Umoja wa Mataifa waanza mazungumzo kuhusu mkataba unaohusu wahamiaji

Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, isipokua Marekani, zimezindua mazungumzo ya muda mrefu leo Jumanne ili kufikia makubaliano na kusainiwa mwezi Desemba nchini Morocco kuhusu Mkataba wa kimataifa juu ya wahamiaji.

Wahamiaji waliokamatwa Sabratha wasafirishwa katika kituo kimoja, Oktoba 7, 2017.
Wahamiaji waliokamatwa Sabratha wasafirishwa katika kituo kimoja, Oktoba 7, 2017. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Suala la wahamiaji linaonekana kama changamoto kubwa duniani.

Vikao sita vya mazungumzo mjini New York, vimepangwa kufanyika hadi mwezi Julai. Lengo ni kufikia makubaliano ambayo yataidhinishwa rasmi tarehe 10 na 11 Desemba katika mkutano wa kilele nchini Morocco, kulingana na wanadiplomasia.

Lengo ni "kuongeza ushirikiano juu ya suala la uhamiaji wa kimataifa kwa vipimo vyake vyote," nakala ya kurasa 25 ya "Mkataba wa Jumla kuhusu wahamiaji".

"Ni muhimu kwamba uhamiaji wa kimataifa utuuunganishe badala ya kutugawa," nakala ya rasimu hiyo pia inasisitiza.

Marekani, ambayo ina uhusiano tata, hasa na Mexico juu ya suala hili la wahamiaji, ilitangaza mwishoni mwa mwaka 2017 kujiondoka mchakato wa kuandaa Mkataba huo kwa sababu ya vipengele vilivyo kinyume na sera mpya ya uhamiaji ya Rais Donald Trump.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.