Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA

Hali ya hatari yatangazwa tena nchini Ethiopia

Hali ya hatari imetangazwa nchini Ethiopia baada ya kujiuzulu kwa Waziri Mkuu Hailemariam Desalegn wiki hii, kwa kile alichokisema anataka kuwa mmoja wa watu watakaoleta suluhu ya kisiasa nchini bumo.

Waandamanaji wa kabila la Oromo nchini Ethiopia wakiandamana katika siku zilizopita
Waandamanaji wa kabila la Oromo nchini Ethiopia wakiandamana katika siku zilizopita Reuters/D Zammit
Matangazo ya kibiashara

Uamuzi huu umeamuliwa na Baraza la Mawaziri, baada ya kukutana kwa dharura jijini Addis Ababa.

Haijafahamika hali hiyo itaendelea hadi lini. Inakuwa mara ya pili kwa Ethiopia kujikuta katika hali hii tangu mwaka 2016.

Serikali jijini Addis Ababa imekuwa ikisema imekuwa ikichukua uamuzi huu kutokana na makabiliano ya kikabila nchini humo na sababu zingine za kiusalama.

Uamuzi huu huenda ukasababisha maandamano zaidi nchini humo kwa sababu, ndio sababu kubwa ambayo imeendelea kuzua makabiliano kati ya waandamanaji na maafisa wa usalama.

Siku ya Ijumaa, wanasiasa wa upinzani walisema raia wa Ethiopia wasitarajie mabadiliko yoyote hata baada ya kujizulu kwa Waziri Mkuu Desalegn.

Chama tawala nchini humo, kitakutana hivi karibuni kujadili hatua ya Desalegn na kumchagua Waziri Mkuu mpya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.