Pata taarifa kuu
LIBERIA SENEGAL-USHIRIKIANO

George Weah azuru Senegal

Rais wa Liberia George Weah anafanya ziara yake ya kwanza ya siku moja nchini Senegal, ziara ambayo ni ya kiserikali na kirafiri.

Rais wa Liberia George Weah (kushoto) akipokelewa na mwenyeji wake wa Senegal Macky Sall tarehe 15 Februari 2018, huko Dakar.
Rais wa Liberia George Weah (kushoto) akipokelewa na mwenyeji wake wa Senegal Macky Sall tarehe 15 Februari 2018, huko Dakar. SEYLLOU / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ziara hii ya Rais Weah nchini Senegal ni katika kumshukuru Macky Sall, ambaye ni mtu wake wa karibu na amekua akipata nasaha nyingi kutoka kwake kabla ya uchaguzi. Ushirikiano kati ya nchi hizo mbili kwa sasa si wa kuridhisha.

Kabla ya kuchaguliwa, nyota wa zamani wa mpira wa miguu alikutana mara kadhaa na Macky Sall kwa mashauriano. Ziara yake wa kwanza rasmi nje ya Liberia, George Weah aliianzia Senegal, kama ishara ya kushukuru lakini pia kuborsha ushirikiano. "Nilipoanza kazi yangu, mara nyingi nilikua nikitokea Dakar kumuona kaka yangu Macky Sall. Leo, nimekua rasmi kama rais wa Jamhuri. Uhusiano wetu utakuepo kusaidia wananchi wa Liberia. Nchi ya Senegal ni mfano.

George Weah hatafuti tuu mfano huo wa senegal lakini pia uungwaji mkono. Kati ya nchi yake na Senegal, ushirikiano huo unaweza kuchukua mfano wa misaada ya mafunzo kwa wanafunzi wa Liberia ambao wataendeleza masomo yao huko Dakar. "Vipaumbele ambavyo ameweka ni masuala ya mafunzo ya ufundi na ujasiriamali. Kwa hili, Senegal ina uzoefu mkubwa ambao tunaweza kushiriki, "amesema Rais wa Senegal Macky Sall.

Ushirikiano ambao unaweza kupanuliwa kwa rasilimali za asili. Senegal na Liberia ni nchi mbili za pwani maarufu kwa rasilimali zao za uvuvi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.