Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mashambulizi ya Ufaransa dhidi ya Ansar Dine yaua watu 10 Mali

Wapiganaji wasiopungua 10 wa kundi la wapiganaji wa Kiislamu la Ansar Dine wameuawa katika mashambulizi ya anga ya jeshi la Ufaransa wakati wa operesheni iliyokua ikimlenga kiongozi wa kundi hilo, Iyad Ag Ghaly Mali, vyanzo vya usalama vimethibitisha.

Wapiganaji wa Ansar Dine karibu na mji wa Kidal, Julai 9, 2012.
Wapiganaji wa Ansar Dine karibu na mji wa Kidal, Julai 9, 2012. AFP/YouTube
Matangazo ya kibiashara

Mshirika wa karibu wa kiongozi huyo, afisa wa zamani aliyetoroka jeshi la Mali, aliuawa katika mashambulizi hayo, jeshi la Mali (FAMA) lilibaini Jumatano usiku.

"Makao makuu ya kiongozi wakundi la Ansar Dine, Iyad Ag Ghaly, yanayopatikana katika eneo la Tinzaouatène yalilengwa katika operesheni hiyo, " chanzo cha usalama kumeliambia Shirika la Habari la AFP kigeni chanzo usalama sasa katika Mali.

Operesheni ya Jumatano ilifanyika "karibu na eneo la Inaghalawass, mita 900 kutoka kwenye mpaka wa Algeria," chanzo hicho ambacho hakikutaja jina lake kimesema.

Ansar Dine, washirika wa Al Qaeda, ni sehemu ya makundi ya waasi yanayodhibiti eneo la kaskazini mwa Mali kati ya mwaka 2012 na Januari 2013. Mnamo mwaka 2015, baada ya kikosi cha Ufaransa cha Barkhane "kutokomeza" (kuua au kukamata) mamia ya wapiganaji wa Kiislamu kaskazini mwa Mali, Iyad Ag Ghaly alikimbilia kwenye mpaka wa Algeria, kwa mujibu wa vyanzo vya kijeshi.

Ripoti iliyotolewa inabaini kwamba wapiganaji wa Ansar Dine kati ya 10 hadi 17 waliuawa katika mapigano hayo, kulingana na chanzo cha usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.