Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MORGAN-SIASA-KIFO

Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai afariki dunia

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe MDC, Morgan Tsvangirai amefariki dunia baada ya kuugua muda mrefu Saratani ya utumbo.

Morgan Tsvangirai katika Kongamano la MDC, Harare mnamo Oktoba 31, 2014.
Morgan Tsvangirai katika Kongamano la MDC, Harare mnamo Oktoba 31, 2014. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Kiongozi huyo wa kihistoria aliyesumbuliwa na Saratani ya utumbo kwa muda wa miaka miwili alifariki jana Jumatano usiku, Februari 14 katika hospitali ya mjini Johannesburg. Kifo chake kimetangazwa kwenye Twitter na Naibu kiongozi wa chama chake, MDC.

"Marehemu alifariki usiku wa Februar 14, " Bw Elias Mudzuri ameliambia Shirika la Habari la Uingereza Reuters.

Kwa zaidi ya miaka kumi na tano, Morgan Tsvangirai alikua mpinzani wa Robert Mugabe. Tsvangirai aliishi miezi mitatu tu baada ya kujiuzulu kwa Robert Mugabe kama rais wa Zimbabwe.

Morgan Tsvangirai aliendesha vita vya kisiasa na kujiweka kando kabisa na vita vya silaha kwa kumtimua Robert Mugabe.

Morgan Tsvangirai alianzisha chama cha Movement for Democratic Change (MDC) mwaka 2000, na kuanza kutoa changamoto kwa aliye kuwa rais wa nchi hiyo aliyekaa madarakani muda mrefu, Robert Mugabe.

Licha ya kupigwa, kufungwa, Morgan Tsvangirai aliendelea kupambana kisiasa. Manamo mwaka 2008, alishinda duru ya kwanza ya uchaguzi lakini aliamua kuacha na kushiriki duru ya pili kwa kuhofia kuuawa kwa wafuasi wake. Mwaka 2009, alikubali kuwa Waziri mkuu. Toka wakati huo Zimbabwe iliingia katika mgogoro wa kipekee,huku mfumuko wa bei ukifikia 1600%. Baada ya miaka mitano Morgan Tsvangirai aliendelea kushindwa kisiasa kutokana na hali ya afya yake.

Morgan Tsvangirai alitarajiwa kuwa mgombea rasmi kwa tiketi ya chama cha MDC katika uchaguzi wa urais wa mwaka huu akipambana dhidi Rais mteule Emmerson Mnangagwa, aliyemrithi Robert Mugabe. Lakini juma lililopita, Tsvangira aliachia ngazi na kutoa nafasi yake kwa Nelson Chamisa, mmoja kati ya manaibu wake watatu, akionyesha kwamba afya yake imeendelea kudorora. Morgan Tsvangirai anaacha chama chake kikigawanywa na kukabiliwa na malumbano ya ndani kwa miezi kadhaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.