Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 16/12 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 15/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Pande zinazokinzana zaendelea tena na mazungumzo Jumatatu kujaribu kuiondoa Ireland ya Kaskazini katika mkwamo wa kisiasa
 • Mjumbe wa Marekani katika mazungumzo Stephen Biegun afutilia mbali msimamo wowote wa Korea Kaskazini lakini aacha mlango wazi kwa mazungumzo
Afrika

Gambia yarejea tena kwenye Jumuiya ya Madola

media Balozi wa Gambia nchini Uingereza Francis Blain (Kushoto) akiwasilisha maombi kwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Madola Patricia Scotland jijini London thecommonwealth.org

Nchi ya Gambia imerejea tena kwenye Umoja wa nchi za Jumuiya ya  Madola, miaka mitano baada ya rais wa zamani Yahya Jammeh kuiondoa.

Jammeh ambaye aliondoka madarakani mwaka 2017, aliiondoa nchi hiyo baada ya kudai kuwa Jumuiya hiyo ilikuwa ya wakoloni.

Uanachama wa Gambia umekubaliwa tena katika Ofisi ya Jumuiya hiyo jijini London nchini Uingereza.

Baada ya kuingia madarakani,  rais wa sasa Adama Barrow, aliahidi kuirejesha nchi hiyo kwenye Jumuiya hiyo katika harakati za kuimarisha uhusiano wa nchi yake na mataifa ya nje.

Gambia inakuwa nchi ya nne kurejea kwenye Jumuiya hiyo baada ya Afrika Kusini, Pakistan na Fiji katika miaka ya hivi karibuni.

Jumuiya ya nchi za Madola iliundwa mwaka 1931 kwa lengo la kuziunganisha nchi zinazozungumza lugha ya Kiingereza.

Inaundwa na mataifa 52.

Kiongozi wa Jumuiya hiyo  ni Malkia wa Uingereza Bi.Elizabeth wa pili.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana