Pata taarifa kuu
DRC-AFYA-USALAMA

Wagonjwa 12 wajeruhiwa kwa visu katika hospitali Goma

Watu wasiojuliana wamejipenyeza katika hospitali maarufu katika kata ya Ndosho, mjini Goma mashariki mwa Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo na kuwachoma visu wagonjwa 12 wakiwa wodini.

Hospitali ya mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 2016.
Hospitali ya mkoa wa Kivu Kaskazini, Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Julai 2016. RFI/Leonora Baumann
Matangazo ya kibiashara

Katika mahojiano maalum na idhaa hii waziri wa afya katika jimbo la Kivu ya kaskazini Dokta Martial Kambumbu amethibitisha kuwa ni tukio ambalo lilifanyika usiku wa jana Jumatatu kuamkia leo Jumanne ambapo majambazi hao walivivamia vituo viwili vya afya nje kidogo ya jiji la Goma, ambako walianza kuwachoma visu wagonjwa ambao walikuwa wamelazwa wakipewa matibabu,

Pamoja na kukiri kuwa majeruhi hao wanaendelea vizuri waziri Kambumbu ameongeza kuwa watatu kati ya wagonjwa hao wako mahututi.

Mashirika ya kiraia katika mji huo wa Goma yanasema hali hiyo imezusha hofu ya kuwepo kwa waasi wa Uganda wa ADF wanaouwa watu kwa kutumia visu katika maeneo ya Beni na viunga vyake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.