sikiliza tena
Mtazamo Wako Kwa Yaliyojiri Wiki Hii
Matukio tuliyoyapa uzito wiki hii duniani
Rais wa DRC Felix Tshisekedi
 
Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/05 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Haraka
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May atangaza kujiuzulu
Afrika

Upinzani waapa kuendelea na maandamno Togo

media Nchini Togo, upinzani umekua ukiandamana kwa miezi kadhaa kushinikiza kumalizika kwa uongozi wa miaka 50 wa familia ya rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe MATTEO FRASCHINI KOFFI / AFP

Upinzani nchini Togo umesema utaendelea kuandamana kuhakikisha rais wa nchi hiyo Faure Gnansigbe anaachia ngazi. Tangu kuzuka kwa maandamno hayo watu kadhaa wamepotza maisha na wengine kujeruhiwa.

Mwandishi wa RFI aliyeko Lome anasema ghasia kubwa zilishuhudiwa jana Jumatano katika nchi nzima kufuatia kile Upinzani unaoundwa na vyama 14 vya kisiasa ulisema kupinga mapendekezo yote yaliyotolewa na serikali ya kutaka kufanyika maridhiano ya kitaifa katika kumaliza mgogoro wa kisiasa uliopo hivi sasa.

Upinzani Umeendelea kuweka shinikizo kwa ajili ya kufanyika mazungumzo ya kisiasa na mageuzi ndani ya serikali iliyoko madarakani.

Upinzani umekua ukiandamana kwa miezi kadhaa kushinikiza kumalizika kwa uongozi wa miaka 50 wa familia ya rais wa nchi hiyo Faure Gnassingbe lakini pia wanapinga kubadilishwa kwa Katiba kwa lengo la kumsaidia rais wa sasa kuendelea kukaa madarakani.

Hata hivyo upinzani umeapa kuendelea na maandamano, huku ukishtumu polisi kutumiwa na chama tawala kwa kusababisha vifo na vurugu nchi nzima.

Upinzani umeomba vyombo vya sheria kuwafikisha mahakamani polisi waliohusika na vifo vya waandamanaji nchini humo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana