Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

Kesi ya mauaji ya rais Kabila yaendelea kuzua utata DRC

Tume ya Afrika ya haki za binadamu imesema inasikitishwa na namna ambavyo kesi ya mauaji ya aliyekuwa rais wa jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Laurent Desire Kabila imekuwa ikiendeshwa.

Hayati rais Laurent-Désiré Kabilaaliuawa Januari 16, 2001 (Hapa ilikua mnamo mwezi Agosti 2000).
Hayati rais Laurent-Désiré Kabilaaliuawa Januari 16, 2001 (Hapa ilikua mnamo mwezi Agosti 2000). YOAV LEMMER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miaka kumi na tano iliyopita, tangu kufunguliwa kwa kesi hiyo miongoni mwa washukiwa 51 wa mauaji hayo, watu 30 wamehukumiwa adhabu ya kifo, miongoni mwao Eddy Kapend Ambaye alikuwa mtu wa karibu wa hayati rais Kabila.

Kwa mujibu wa Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu wafungwa wengine kati ya watuhumiwa hawana hatia, na tangu mwaka 2013 imekuwa ikiomba waachiwe huru.

Rais Laurent Desire Kabila aliuawa kwa kupigwa risasi tarehe 16 Januri 2001 katika ikulu mjini Kinshasa.

Baadhi wanasema rais Kabila aliuawa na mtu wake wa karibu, huku wengine wakimshtumu Eddy Kapend kuwa ndie alihusika na kifo cha Kabila.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.