Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Wakuu wa Afrika wanamalizia mkutano wa siku mbili jijini Addis Ababa

media Mwenyekiti mpya wa Umoja wa Afrika Rais Paul Kagame wa Rwanda Januari 28 2018 SIMON MAINA/AFP

Mkutano wa siku mbili wa wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika unamalizika siku ya Jumatatu jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Wakuu hao wa bara Afrika walianza kukutana mwishoni mwa wiki iliyopita, kujadili masuala mbalimbali yanayowasumbua waafrika kama ukosefu wa usalama na uchumi.

Kauli mbinu ya mwaka 2018 wa Umoja huo ni namna ya kupambana na ufisadi. Rais wa Nigeria Muhamadu Buhari amepewa jukumu la kusimamia juhudi za kupambana na ufisadi.

Buhari tangu kuchaguliwa kwake mwaka 2015, amekuwa akisfiwa sana katika vita dhidi ya ufisadi katika nchi yake.

Mwenyekiti mpya wa Umoja huo rais wa Rwanda Paul Kagame, ametoa wito kwa wakuu wa nchi za Afrika kufungua mipaka yake, ili kuwaruhusu waafrika kutembea bila vikwazo.

Rwanda imekuwa nchi ya kwanza barani Afrika, kuondoa vikwazo vya kuingia nchini mwake kwa lengo la kuhimiza Umoja wa Afrika. AU inataka kuondoa mipaka na kuungana kisiasa kufikia 1963.

Aidha, Kagame anataka teknolojia kutumiwa vema ili kusaidia kuunda nafasi za kazi hasa kwa vijana.

Suala la namna bara la Afrika linavyoweza kujitegemea kwa kupata fedha zake bila ya kutegemea misaada kutoka mataifa ya nje.

Mbali na viongozi wa Afrika, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress na kiongozi wa Palestina Mahmoud Abbas wamehudhuria mkutano huo.

Guteress ametaka ushirkiano wa karibu na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali barani Afrika hasa usalama huku Abbas akitaka mataifa ya Afrika kuendelea kuwaunga mkono Wapalestina hasa wakati huu ambao Marekani imeamua kutambua Jerusalem kuwa makao makuu ya Israel.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana