Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Serikali ya Congo-Brazzaville yakutana kwa mazungumzo na waasi

media Katikati mwa mji mkuu wa Congo, Brazzaville. Serikali imekutana kwa mazungumzo na waasi wanaoongozwa na Frederic Bintsamou. Wikimedia

Serikali ya Congo-Brazzaville yakutana kwa mazungumzo na waasi Kwa mara ya kwanza Serikali ya Congo-Brazzaville imekutana kwa mazungumzo na wajumbe wa kundi la waasi jana Jumatano tangu kusitisha mapigano yaliyogharimu maisha ya mamia ya wakaaji wa eneo la Pool.

Kundi hili la waasi linaloongozwa na mkuu wa zamani wa majeshi ya nchi hiyo, Frederic Bintsamou. Mkataba wa kwanza wa amani kati ya serikali na kundi hili uliosainiwa mwaka 2003.

Ambapo mwezi Aprili mwaka jana walipigana na jeshi la serikali ya nchi hiyo wakisema kuwa wanapinga matokeo ya uchaguzi wa hivi karibuni uliompa ushindi Rais Denis Sassou Nguesso.

Hayo yanajiri siku tatu baada ya afisa mmoja wa juu wa jeshi la Congo ambaye pia alikuwa mtu wa karibu wa rais Denis Sassou Nguesso kukamatwa jijini Brazzaville akituhumiwa kupanga njama za kutaka kuipindua Serikali.

Jenerali Norbert Dabira alikamatwa siku ya Jumatano ya wiki hii na polisi na toka wakati huo amekuwa akihojiwa na kikosi maalumu ya idara ya usalama wa taifa.

Afisa mmoja wa jeshi ambaye hakupenda kutaja jina lake alisema kuwa tuhuma dhidi ya Dabira zinahusu jaribio analodaiwa kuwa alilipanga mwaka 2017 kumpindua rais Sassous Nguesso.

Kukamatwa kwa Jenerali Dabira kunakuja wakati huu ambapo Serikali inawatuhumu wanasiasa wa upinzani kwa kujaribu kuhatarisha usalama wa taifa na kuzusha vurugu ambapo mpaka sasa wanasiasa kadhaa wanashikiliwa.

Watu wengine wanaoshikiliwa sambamba na Jenerali Dabira ni pamoja na aliyekuwa mkuu wa utawala wa jeshi la nchi hiyo Jenerali Jean-Marie Michel Mokoko na waziri wa zamani Andre Okombi Salissa ambao wote waligombea urais mwaka 2016.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana