Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-CENCO

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC watangaza maandamano mapya dhidi ya rais Kabila

Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wameitisha maandamano mapya dhidi ya rais Joseph Kabila, kumshinikiza aondoke madarakani na kutangaza kuwa hatawania urais mwezi Desemba mwaka 2018.

Maandamano jijini Kinshasa Desemba 31 2017 jijini Kinshasa
Maandamano jijini Kinshasa Desemba 31 2017 jijini Kinshasa John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Maandamano haya mapya, yamepangwa kufanyika tarehe 21 mwezi huu katika miji mbalimbali nchini humo.

Hatua hii imekuja baada ya maandamano mengine kufanyika, mwishoni mwa mwaka uliopita na kusababisha vifo vya waandamanaji saba baada ya makabiliano kati ya polisi na waandamanaji.

Maaskofu wa Kanisa Katoliki wamesema, hawatachoka kushinikiza mabadiliko nchini DRC, na kumshinikiza rais Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 kuondoka madarakani na kutowania urais mwishoni mwa mwaka huu.

Siku ya Ijumaa, Maaskofu hao waliongoza ibada ya kuwakumbuka watu waliopoteza maisha katika maandamano yaliyopita na kutoa wito kwa raia wa nchi hiyo kutokata tamaa katika harakati hizo.

Polisi wa kupambana na ghasi walikabiliana na wauamini wa Kanisa hilo waliokuwa wamemaliza ibada hiyo na kusababisha baadhi yao kujeruhiwa kwa hofu kuwa wangeandamana jijini Kinshasa.

Rais Kabila hajajitokeza kusema iwapo atawania tena au la licha ya shinikizo anazoendelea kupata.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.