Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Watu 10 watekwa nyara Beni, DRC

media Wanajeshi wa Serikali ya DRC, wakiwa kwenye misitu ya Beni mashariki mwa DRC kuwasaka wapiganaji wa waasi wa Uganda, ADF ambao wanatekeleza mauaji ya kiholela UN Photo/Sylvain Liechti

Watu waliokuwa wamejihami kwa silaha wameripotiwa kuwateka nyara watu zaidi ya 10 kwenye mji wa Beni mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Miongoni mwa waliotekwa ni mkurugenzi wa radio washirika wa RFI, RTGB Beni ambayo huwa inajiunga na matangazo yetu ya Kiswahili.

Mashuhuda wanasema watu hao walikuwa wamevalia sare za kijeshi ambapo baadae walitokemea na mateka wao kusikojulikana baada ya kuwapora kila walichokuwa nacho.

Makundi ya waasi wakiwemo Mai-Mai na kundi la ADF yamekuwa yakiyumbisha usalama kila uchao katika maeneo hayo kiasi kwamba hadi sasa ni vigumu kubaini wahusika.

 kundi la waasi wa Uganda linaloendesha harakati zake mashariki mwa DRC, limewaua mami ya watu katika maeneo mmbalimbali jirani na mji wa Beni.

Hivi karibuni jeshi la Uganda (UDF) likishirikiana na jeshi la DRC, (FARDC) liliendesha operesheni kabambe mashariki mwa DRC dhidi ya kundi hili.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana