Pata taarifa kuu
DRC-ICC-BEMBA-HAKI

Kesi ya Jean-Pierre Bemba yaendelea kusikilizwa ICC

Kesi ya rufaa, iliyowasilishwa na aliyekuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jean-Pierre Bemba, inatarajiwa kumalizika siku ya Jumatatu.

Makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba akutwa na hatia ya makosa 5 ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.
Makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba akutwa na hatia ya makosa 5 ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Kesi ya Bemba ilianza kusikilizwa wiki hii, baada ya Mawakili wake kusema kuwa hawakuridhika kamwe na hukumu iliyotolewa dhidi ya mteja wake, na kuwatuhumu Majaji kwa kupuuza ushahidi wa utetezi wao.

Bemba alihukumiwa jela miaka 18 jela mwaka 2016, baada ya kupatikana na makosa ya uhalifu dhidi ya binadamu, mauaji na ubakaji.

Majaji wa ICC walibaini kuwa, Bemba aliamuru kundi la wapigananaji wake ALC, wapatao 1,500 nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kuisaidia serikali ya nchi hiyo katika vita dhidi ya vikosi vya upinzani.

Wakiwa katika nchi jirani, Bemba alipatikana na kosa la kuwaagiza wapiganaji wake kuwauawa, kuwabaka wasichana na wasicha pamoja na kuvamia na kupora mali za watu wasiokuwa na hatia.

Bemba ambaye kabla ya hukumu yake, alikuwa anazuiwa tangu mwaka 2008. Hajawahi kukiri tuhma dhidi yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.