Pata taarifa kuu
MALI-LIBYA-WAHAMIAJI

Mali yaomboleza vifo vya raia wake 48 waliokufa maji Libya

Serikali ya Mali imetangaza siku 2 za maombolezo ya kitaifa kutokana na vifo vya raia wake 48 waliopoteza maisha kwenye bahari ya pwani ya Libya wakijaribu kuingia barani Ulaya mwishoni mwa juma lililopita.

Wahamiaji waliokolewa na kikosi cha ulinzi wa baharini cha Libya, Januari 9, 2018.
Wahamiaji waliokolewa na kikosi cha ulinzi wa baharini cha Libya, Januari 9, 2018. REUTERS/Hani Amara
Matangazo ya kibiashara

Kwa siku mbili hizo, bendera nchini kote zitapandishwa nusu mlingoti, kwa mujibu wa taarifa ya serikali ya Mali.

Kati ya wahamiaji 90 na 100 walitoweka baharini baada ya boti lao kuzama kwenye pwani ya Libya, Jenerali Ayoub Kacem, msemaji wa kikosi cha wanamaji cha Libya alisema siku ya Jumanne jioni.

Ndoto yao ilikua kwenda Ulaya lakini imeishia baharini. Kwa mujibu wa Jenerali Kacem, akinukuu watu walionusurika katika tukio hilo, boti hilo lilikua likibeba watu zaidi ya 100. 17 pekee, ikiwa ni pamoja na wanawake, ndio waliokolewa.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, tukio hilo lilitokea kwenye pwani ya mji wa al-Khoms, kilomita mia moja mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Kikosi cha wanamaji cha Libya kimeongeza kuwa kiliokoa wahamiaji wengine 267 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa katika boti mbili kwenye pwani ya mji wa Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa Tripoli.

Wanawake na watoto ni miongoni mwa wahamiaji waliokolewa, amesema jenerali Kacem,

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wahamiaji kumi walikufa maji na wengine zaidi ya 50, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo, walitoweka katika pwani ya Libya, kulingana na ripoti iliyokusanywa na mashirika kadhaa kutoka kwa waathirika. Mnamo mwaka 2017, wahamiaji 3116 walikufa maji au walitoweka wakati walipo kuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya, ikiwa ni pamoja na 2833 kwenye pwani ya Libya, kulingana na ripoti ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Lakini jaribio la kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya limepungua kwa kasi tangu majira ya joto, baada ya jitihada za Italia kuzuia wahamiaji kusafiri kwenda Ulaya wakitumia bahari ya Mediterranean, kufuatia makubaliano na mamlaka ya Libya na wanamgambo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.