Cote d'Ivoire yasikitishwa na uvamizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Bouake
Kambi moja ya jeshi kwenye mji wa Bouake nchini Cote d'Ivoire ambako mwaka jana kulishuhudiwa uasi wa wanajeshi, imevamiwa na kuharibiwa na wanajeshi wa Serikali.
Imechapishwa:
Milio ya risasi ilisikika Jumanne usiku kwenye kambi hiyo wakati wanajeshi kutoka kambi nyingine walipovamia kambi hiyo yenye wanajeshi wa kikosi maalumu na kuanza kuharibu ofisi na kuchoma moto magari.
Msemaji wa Serikali ya Cote d'Ivoire, Bruno Kornee, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa, hali ya utulivu tayari imerejea kwenye mji huo.
Tukio hili jipya lilijadiliwa katika kikao cha Baraza la Mawaziri cha siku ya Jumatano, Januari 10. Mawaziri wote walielezea masikitiko yao kutokanna na uvamizi huo.
Hivi karibuni rais Allasane Ouattara alitangaza kuanza kutekeleza mabadiliko ya kuwapunguza mamia ya wanajeshi waasi waliomsaidia kuingia madarakani ili kutengeneza jeshi la kitaifa hatua ambayo imezusha hofu ya kutokea uasi mwingine.