Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 12/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 11/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
  • Macron aahirisha mkutano wa kilele wa Pau kuhusu Sahel hadi mwanzoni mwa mwaka 2020 kwa sababu ya shambulio nchini Niger (Elysee)
Afrika

Wahamiaji 100 watoweka baharini pwani ya Libya

media Wahamiaji wakiokolewa na meli ya kikosi cha ulinzi wa bahari cha Libya, wakiwasili kwenye bandari ya Tripoli, Novemba 2017. REUTERS/Ahmed Jadallah

Kati ya wahamiaji 90 na 100 wametoweka baharini baada ya boti lao kuzama kwenye pwani ya Libya, Jenerali Ayoub Kacem, msemaji wa kikosi cha wanamaji cha Libya alisema siku ya Jumanne jioni.

Ndoto yao ilikua kwenda Ulaya lakini imeishia baharini. Kwa mujibu wa Jenerali Kacem, akinukuu watu walionusurika katika tukio hilo, boti hilo lilikua likibeba watu zaidi ya 100. 17 pekee, ikiwa ni pamoja na wanawake, ndio waliokolewa.

Kwa mujibu wa chanzo cha kijeshi, tukio hilo lilitokea kwenye pwani ya mji wa al-Khoms, kilomita mia moja mashariki mwa mji mkuu wa Libya, Tripoli.

Kikosi cha wanamaji cha Libya kimeongeza kuwa kiliokoa wahamiaji wengine 267 kutoka nchi mbalimbali za Afrika waliokuwa katika boti mbili kwenye pwani ya mji wa Zawiya, kilomita 50 magharibi mwa Tripoli.

Wanawake na watoto ni miongoni mwa wahamiaji waliokolewa, amesema jenerali Kacem, akisikitishwa na ukosefu wa uwezo na hali mbaya ya hewa ambayo ilivuruga zoezi la uokoaji.

Wahamiaji 3116 walikufa mwaka 2017

Mwishoni mwa wiki iliyopita, wahamiaji kumi walikufa maji na wengine zaidi ya 50, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo, walitoweka katika pwani ya Libya, kulingana na ripoti iliyokusanywa na mashirika kadhaa kutoka kwa waathirika. Mnamo mwaka 2017, wahamiaji 3116 walikufa maji au walitoweka wakati walipo kuwa wakijaribu kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya, ikiwa ni pamoja na 2833 kwenye pwani ya Libya, kulingana na ripoti ya Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

Lakini jaribio la kuvuka bahari ya Mediterranean kuelekea Ulaya limepungua kwa kasi tangu majira ya joto, baada ya jitihada za Italia kuzuia wahamiaji kusafiri kwenda Ulaya wakitumia bahari ya Mediterranean, kufuatia makubaliano na mamlaka ya Libya na wanamgambo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana