Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/08 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/08 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Kesi ya Bemba kusikilizwa katika mahakama ya Rufaa ICC

media Makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba akutwa na hatia ya makosa 5 ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu. AFP/MICHAEL KOOREN

Kesi ya Jean-Pierre Bemba, makamu wa zamani wa rais nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kiongozi wa chama cha upinzani cha MLC, inatarajia kuanza kusikilizwa leo Jumatano Januari 10 katika Kitengo cha Rufaa cha ICC mjini Hague, Uswisi.

Kuanza kwa kesi hii ni ombi la wanasheria wa wa Bemba na wa ofisi ya mwendesha mashitaka.

Mawakili wa makamu wa rais wa zamani wa DRC Jean-Pierre Bemba wamekashifu hukumu ya makosa ya kivita dhidi ya mteja wao, wakiwatuhumu majaji wa mahakama ya ICC kwa kutozingatia ushahidi ambapo, wametoa wito kwa hukumu hiyo kutupiliwa mbali.

Bemba alikata rufaa kupinga hukumu ya kifungo cha miaka 18 jela iliyotolewa na mahakama hiyo mwezi Juni 2016 baada ya kukutwa na hatia ya makosa 5 ya kivita na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na vikosi vyake kuhusika kutekeleza mauaji nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mahakama hiyo ilidai Bemba alishindwa kuzuia vitendo vya ubakaji na mauaji vilivyotekelezwa na wanajeshi wake kati ya mwaka 2002 na 2003.

Mpaka sasa viongozi wa kivita wasiopungua watatu kutoka DRC , Jean-Pierre Bemba, Thomas Lubanga na Bosco Ntagandandio wanazuiliwa na Mahakama ya ICC kwa makosa ya kivita.

Hivi karibuni Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) iliweka kiwango cha dola milioni 10 kwa malipo ya pamoja ya askari watoto waliolazimishwa kujiunga na kundi la zamani la wanamgambo lililoongozwa na Thomas Lubanga.

Mahakama "imeweka kiwango hicho kama fidia ambayo Bw Lubanga anatakiwa kulipa kwa waathirika 425 waliochukuliwa kama ushahidi na kuhusika kwake kwa kutowatendea haki waathirika wengine, "alisema Jaji Marc Perrin de Brichambaut.

Thomas Lubanga wakati huo kiongozi wa kundi la waasi la UPC, ambaye alihukumiwa miaka kumi na nne jela, alipatikana na hatia mwaka 2012 ya kuajiri watoto, ikiwa ni pamoja na watoto wenye umri wa miaka kumi na mmoja, na kuwatumia kama askari au walinzi mwaka 2002 na 2003 katika eneo la Ituri, kaskazini-mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Naye aliyekuwa kiongozi wa kundi la waasi la FPLC nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Bosco Ntaganda, maarufu kama "The Terminator" amekuwa akikanusha madai kuwa aliwatumia watoto wadogo kama wapiganaji na kuwatumia wanawake na wasichana kama watumwa wa kingono.

Kesi dhidi ya Ntanganda ilianza miaka miwili iliyopita mjini Hague nchini Uholanzi, alipofunguliwa mashtaka ya mauaji katika jimbo la Ituri yaliyotokea kati ya mwaka 2002 na 2003.

Watu zaidi ya 60,000 walipoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao baada ya kuvamiwa na waasi hao.

Kabla ya kufikishwa katika Mahakama ya ICC, Ntaganda alijisalimisha katika Ubalozi wa Marekani jijini Kigali  nchini Rwanda mwaka 2013.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana