Pata taarifa kuu
LIBYA-ULAYA-WAHAMIAJI

Wahamiaji 290 waokolewa kwenye pwani ya Libya

Wanawake wawili wamepoteza maisha na wahamiaji zaidi ya 290 wameokolewa kutoka katika boti mbili walizokuwa wakisafiria kwenye pwani ya bahari ya Libya, jeshi la nchi hiyo limethibitisha.

Wahamiaji wakiwa katika boti kwenye pwani ya Libya wakisubiri kuokolewa Agosti 2,2017.
Wahamiaji wakiwa katika boti kwenye pwani ya Libya wakisubiri kuokolewa Agosti 2,2017. Angelos Tzortzinis / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao waliokolewa kutoka kwenye pwani ya Garabulli iliyo umbali wa kilometa 50 na mji wa tripoli na kisha baadae walichukuliwa hadi kwenye kambi maalumu ya mjini Tripoli.

Kwa mujibu wa jeshi wahamiaji hao waliondoka kwenye pwani ya Libya majira ya alfajiri kwa kutumia boti iliyokuwa na watu 140 kutoka kwenye mataifa mbalimbali ya Afrika lakini injini ya boti yao iliharibika na kuanza kupoteza uelekeo.

Jeshi linasema wahamiaji wengine 150 walikuwa kwenye boti ya pili ambayo na yenyewe ilikuwa inaelekea kuzama kabla ya kuwakoa.

Tangu kuanguka kwa utawala wa Marehemu Kanali Muamar Gadafi nchi ya Libya imekuwa kitovu cha biashara ya binadamu licha ya juhudi za nchi za Ulaya kutaka kuizuia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.