Pata taarifa kuu
DRC-HAKI

Serikali ya DRC yaendelea kuwashikilia wanaharakati wa Filimbi

Wakili wa wafuasi wa vuguvugu la Filimbi nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ameitaka serikali kuwaachia huru bila masharti wanaharakati wa vuguvugu hilo waliotiwa nguvuni tangu Desemba 30 mwaka uliiopita wakati wakiwa katika harakati za kuhamasisha wananchi kuitikia maandamano yalioitishwa na kanisa Katoliki.

Wanaharakati wa vuguvugu Filimbi wakijitayarisha kushiriki maandamano Kinshasa mnamo Oktoba 29.
Wanaharakati wa vuguvugu Filimbi wakijitayarisha kushiriki maandamano Kinshasa mnamo Oktoba 29. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Wakili Kabé amesema anatiwa wasiwasi na kuendelea kuzuiliwa kwa Karbone Beni, mratibu wa vuguvugu la Filimbi linalotetea mageuzi, pamoja na wanachama wengine wanne ambao wanatuhumiwa kumkashifu rais wa jamuhuri pamoja na uchochezi.

Kwa upande wake msemaji w a Serikali ya DRC ambaye pia ni Waziri wa habari Lambert Mende, amewataka mawakili wa watuhumiwa hao kufungua kesi mahakamani iwapo wanaona wateja wao wameonewa.

Haya yanajiri wakati huu ambapo mwishoni mwa juma umoja wa Mataifa uliikashifu vikali Serikali ya DRC kwa namna ambavyo inaendesha operesheni dhidi ya viongozi wa upinzani na raia walioshiriki maandamano ya juma moja lililopita kushinikiza raus Joseph Kabila kuondoka madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.