Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/07 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/07 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Senegal yaomboleza vifo vya raia wake 13 waliouawa

media Misitu ya Casamance,Senegal ni maeneo yenye utajiri. Mathieu Damman/Wikimedia Commons

Serikali ya Senegal mwishoni mwa juma imeapa kutokuwa na huruma katika msako wake wa kujaribu kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria watu waliohusika na mauaji ya raia 13 kusini mwa nchi hiyo kwenye mji wa Casamance.

Watu waliokuwa na bunduki waliwashambulia kundi la wanaume na vijana waliokuwa wanatafuta kuni na kisha kuwaambia walale chini kabla ya kuwafyatulia risasi, hili likiwa ni tukio baya kuripotiwa kwenye mji huo kwa miaka.

Rais Macky Sall amelaani tukio hilo na kuitisha kikao cha baraza la usalama.

Haijulikani waliohusika na uhalifu huo. Kinachoeleweka tu ni kwamba hali ni ya kutatanisha karibu na misitu ya Casamance.

Kesi hii inaonekana ni ulipizaji kisase kati yawanakijiji na wauzaji haramu wa kuni katika msitu wa Toubacouta,kulingana na ushuhuda uliokusanywa katika eneo la tukio. Vijana wa Toubacouta ndio walikabidhiwa ulinzi wa msitu huo na wamekua wakitoza kodi kwa kila mti.

"Wanachama wa kamati hii inaojumuisha vijana wanaolinda msitu wa Toubacouta pia ni wafanyabiasha haramu wa kuni au miti kama sisi," amesema kijana alienusurika wakati wa mauaji hayo. Wao ndio ambao wanatuuzia miti hiyo, kwa zaidi ya miaka 20, kila mtu anajua hilo. Tunalipa frannga za CFA 10,000 kwa leseni na franga za CFA 2,500 za mfuko wa kijiji. Hii imeendelea kwa miaka 20. Lakini tangu tulielewa kuwa msitu ni wa kwetu sote, tulikataa kulipa kodi. Hii ndiyo sababu ya kutokuelewana ... "

Kwa hiyo pesa zinakwenda wapi? Je idara ya maji na misitu inafahamu hili? "Wanafahamu vizuri, amejibu kijana huyo. Viongozi wote wanatambuliwa hilo. Lakini wanatuambia kwamba hati inayoolewa na kamati ni muhimu tu katika misitu.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Senegal ameahidi kifunaya kile kilio chini ya uwezo wake ili kuwakamata wahusika wa mauaji ya siku ya Jumamosi. Aly Ngouille Ndiaye amehakikisha kuwa tukio hili halihatarishi mchakato wa amani katika eneo hilo.

Serikali ya Senegal imetangaza maombolezo ya kitaifa ya siku tatu kuanzia leo Jumatatu.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana