Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-TANZANIA

Umoja wa Mataifa kuchunguza mauaji ya wanajeshi wa Tanzania nchini DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametangaza kuwa, Umoja huo utachunguza mauaji ya wanajeshi wa Umoja huo waliouawa mwaka uliopita Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha nchini DRC, miili yao ikirejeshwa nyumbani.
Wanajeshi wa Tanzania waliopoteza maisha nchini DRC, miili yao ikirejeshwa nyumbani. REUTERS/Emmanuel Herman
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi 15 kutoka nchini Tanzania wanaohudumu katika jeshi la Umoja wa Mataifa walipoteza maisha baada ya kushambuliwa na waasi wa ADF NALU wilayani Beni, Mashariki mwa nchi hiyo.

Wengine zaid ya 40, walijeruhiwa na wameendelea kupata matibabu.

Uchunguzi huo wa Umoja wa Mataifa, utalenga kubaini namna shambulizi hilo lilivyotekelezwa lakini pia kuja na mapendekezo ya namna ya kukabiliana na mashambulizi kama haya katika siku zijazo.

Tayari Katibu Mkuu Guteress amemteua, naibu wake Dmitry Titov, kuongoza uchunguzi huo.

Shambulizi dhidi ya wanajeshi wa Umoja wa Mataifa nchini DRC mwaka uliopita, ndilo baya zaidi kuwahi kutokea katika miaka ya hivi karibuni.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.