Pata taarifa kuu
DRC-MAFURIKO

Serikali ya DRC yatangaza siku mbili za maombolezo kuwakumbuka watu waliopoteza maisha

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imetangaza siku mbili za maombolezo kati ya Jumatatu na Jumanne wiki ijayo, kuwakumbuka watu 44 waliopoteza maisha katika mafuriko makubwa yaliyotokea wiki hii jijini Kinshasa.

Athari ya mafuriko jijini Kinshasa nchini DRC
Athari ya mafuriko jijini Kinshasa nchini DRC AFP/John Wessels
Matangazo ya kibiashara

Mbali na mauaji hayo, makaazi ya watu 5,000 yamejaa maji, huku makaazi mengine 192 yakiharibika ikiwa ni pamoja na kuvunjika kwa madaraja na barabara.

Maeneo yaliyoathiriwa zaidi na mafuriko hayo ni pamoja na Ngaliema, Bandalungwa, Barumbu, Limete na Selembao.

Jiji la Kinshasa limeendelea kukabiliwa na mafuriko mara kwa mara mvua inaponyesha kutokana na miundo mbinu mibaya hasa mitaro ya kupitisha  maji na msongamano wa makaazi ya watu.

Maakazi mengi ya watu yamejengwa katika maeneo ya milima, katika eneo hilo lenye watu Milioni 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.