Pata taarifa kuu
DRC-MAANDAMANO-USALAMA

Watu 7 wauawa wakati wa maandamano Kinshasa, DRC

Watu saba waliuawa siku ya Jumapili katika mji wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wakati wa maandamano yaliyoitishwa na viongozi wa Kanisa Katoliki nchini gumo kumtaka tais Kabila aheshimishe makubaliano ya Desemba 31, 2017. Taarifa hii imethibitishwa na chanzo cha Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco.

Waandamanaji wakikimbia polisi, Desemba 31, 2017,  Kinshasa, DRC.
Waandamanaji wakikimbia polisi, Desemba 31, 2017, Kinshasa, DRC. John WESSELS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu saba waliuawa katika mji wa Kinshasa na mmoja katika mji wa Kananga wakati wa maandamano yaliyofanyika kutaka serikali kuheshimu makubaliano ya Saint Sylvestre yalifikiwa Desemba 31, 2017 chini ya mwamvuli wa maasofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC. Makubaliano hayo yalishirikishautawala wa rais Joseph Kabila na sehemu moja ya upinzani. Makubaliano hayo yalitaka Uchaguzi Mkuu kufanyika mwishoni mwa mwaka 2017, wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni kurejea nchini na wafungwa wa kisiasa waachiwe huru.

Taarifa ya kuuawa kwa watu saba mjini Kinshasa imethibitishwa na Tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, Monusco. Hata hivyo msemaji wa serikali, Lambert Mendé amefutilia mbali taarifa hiyo, akibaini kwamba watu wawili pekee ndio walipoteza maisha miongoni mwa waandamanani na polisi mmoja.

Lambert Mendé pia amesema kwamba kulikuwa na watu wenye hasira miongoni mwa waandamanaji, na ndio sababu kulitokea makabiliano yaliosababisha vifo hivyo: "Maandamano yalikua ya amani kweli lakini kuna watu ambao walikua na hasira na walitaka kuzua vurugu kabla ya polisi kuingilia kati. Viongozi wa mji wa Kinshasa walikuwa wamewaonya waandamanaji kutoingia mitaani kwa kuhofia kutokea kwa machafiko, lakini hawakutii amri hiyo. Na sasa angalia jinsi tumepoteza ndugu zetu, " amesema Lambert Mende

Alipoulizwa kuhusu mwendendo wa polisi, msemaji wa serikali hakukataa kuwa baadhi ya polisi au askari waliweza kuwatimua waandamanaji kanisani wakitumia gesi ya machozi: "Ikiwa walikuwa na dalili kwamba kuna wahalifu ambao waliweza kuingia katika maeneo hayo matakatifu, sidhani kwamba polisi wangeiacha kukabiliana na magaidi kwa sababu waliingia kanisani. "

Hatuwezi kulaumu polisi kwa kutumia gesi ya machozi.

Msemaji wa serikali ya DR Congo, Lambert Mende, ameongeza

Hata hivyo viongozi wa Kanisa Katoliki wanasema watu kumi ndio waliuawa na Makasisi kadhaa walikamatwa siku ya Jumapili katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa.

"Tuko hapa tunakabiliwa na mashambulizi makubwa dhidi ya uhuru wa ibada na kuandamana, amesema

Padri Donatien Nsholé, Naibu Katibu Mkuu wa Kwanza wa Baraza la Maaskofu Kanisa Katoliki nchini DRC.

Kabila ambaye amekuwa akiongoza DRC tangu mwaka 2001, na ambaye kwa mujibu wa serikali ya pamoja muda wake unamalizika leo, hajatangaza iwapo hatawania urais mwakani.

Uchaguzi ulikuwa umepangwa kufanyika mwisho wa mwaka 2017, lakini kwa sababu mbalimbali hasa za kiusalama, Tume ya Uchaguzi ikaahirisha hadi mwaka 2018.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.