Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 15/12 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 14/12 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Upinzani kufikisha malalamiko yake mahakamani dhidi ya sheria mpya ya uchaguzi DRC

media Waandamanaji wa upinzani karibu na makazi ya Felix Tshisekedi, kiongozi wa chama cha UDPS, Novemba 30, 2017 Kinshasa, DRC. JUNIOR KANNAH / AFP

Muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC umesema kuwa utakwenda Mahakamani kushinikiza kutupiliwa mbali kwa sheria mpya ya Uchaguzi iliyotiwa saini na rais Jospeh Kabila.

Msemaji wa muungano huo Christophe Lutundula, amesema sheria hiyo ni ya kibaguzi na inalenga kuwazuia baadhi ya wanasiasa kuwania nyadhifa mbalimbali mwaka 2018.

Upinzani unasema wanasiasa waliofungiwa nje ni wagombea binafasi amabo kwa mujibu wa sheria hii mpya, huenda wasipate uungwaji mkono wa kutosha.

Tayari wabunge 50 wamejitokeza kupinga sheria hiyo.

Muungano wa vyama vya upinzani tayari umekusanya zaidi ya saini 50 zinazopinga sheria mpya ya Uchaguzi.

Wakati huo huo Moise Katumbi Chapwe, mmoja wa wanasiasa wa upinzani walio uhamishoni nje ya nchi amewatolea wito raia wa DRC kutomkubalia rais Joseph Kabila kuendelea kuongoza taifa hilo ifikapo Desemba 31.

Amesm aanaunga mkono makubaliano ya kisiasa yaliyoafikiwa mwaka mmoja uliopita chini ya jitihada za Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini DRC, Cenco.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana