Pata taarifa kuu
Chad-SIASA-UASALAMA

Hali ya sintofahamu yaendelea Chad

Upinzani nchini Tchad umesema tatizo lililopo nchini humo sio idadi ya mawaziri bali, ni rais mwenyewe Idriss Déby Itno ambae yupo madarakani kwa kipindi cha miaka 27 bila kuwa na mpango wowote wa maendeleo.

Rais wa Chad Idriss Déby aendelea kukosolewa na upinzani.
Rais wa Chad Idriss Déby aendelea kukosolewa na upinzani. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Haya yanajiri baada ya serikali kutangaza kufanya marekebisho ya baraza la mawaziri kutoka mawaziri 37 hadi 24 huku vigogo kadhaa wakijikuta baadhi wametupwa nje wengine wakibadilishiwa wizara mathalan wizara ya usalama wa raia, ya mambo ya nje na ya sheria.

Serikali inasema hatua hiyo imechukuliuwa ili kupunguza gharama na kukabiliana na mgogoro wa kiuchumi. Upinzani nchini humo unasema hiyo ni serikali isiokuwa na faida yoyote. Mahamat Ahmad Alhado, ambae ni mratibu wa muungano wa upinzani nchini Tchad amesema hali mbaya inayoshuhudiwa nchini Chad inasababishwa na utawala mbaya wa Idriss Déby.

Baraza hilo jipya la mawaziri limeshuhudia mawaziri 18 wakiondoka huku wengine 8 wapya wakijiunga.

Hivi karibuni wafuasi wa upinzani walimiminika mitaani kulalamikia mgogoro wa kijamii unaoikabili nchi hiyo. Muungano wa upinzani, UNDR, Uliitisha maandamano makubwa katika uwanja wa michezo wa N'Djamena, lakini polisi waliwatawanya waandamanaji na kuwazuia kufika uwanjani hapo.

Makabiliano makali yamekua yakishuhudiwa kati ya waandamanaji wa upinzani na polisi nchini Chad.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.