Pata taarifa kuu
ANGOLA

Angola: Shirika la mafuta kumchunguza mtoto wa dos Santos kwa tuhuma za ufisadi

Kampuni ya uma ya mafuta nchini Angola imetangaza kuanzisha uchunguzi kuhusu uwezekano kuwa kulikuwa na ubadhilifu wa fedha za shirika hilo uliofanywa na aliyekuwa mkurugenzi wake Isabel dos Santos, mtoto wa rais wa zamani wa nchi hiyo.

Isabel dos Santos aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la mafuta la Angola na mtoto wa rais dos Santos
Isabel dos Santos aliyekuwa mkurugenzi wa shirika la mafuta la Angola na mtoto wa rais dos Santos REUTERS/Toby Melville
Matangazo ya kibiashara

Katika wiki za hivi karibuni vyombo kadhaa vya habari nchini Angola vimeripoti kuwa dos Santos aliagiza kuhamishwa na kulipwa kwa mamilioni ya fedha kinyume cha sheria.

Dos Santos alichaguliwa na baba yake Jose Eduardo dos Santos mwaka 2016 kuwa mkurugenzi wa shirika la mafuta la uma na nafasi yake ilitenguliwa mwezi uliopita na rais mpya wa Angola Joao Lourenco.

Isabel mwenyewe ameendelea kukanusha kuhusika na wizi au ubadhilifu wowote wakati akiwa mkurugenzi wa shirika hilo.

Msemaji wa shirika la Sonangol, Mateus Benza amesema kuwa “tumeanzisha tume ya uchunguzi wa ndani na taarifa zichapishwe”.

Kwa mujibu wa jarida la Novo Jornal na The Jornal Economico yameripoti kuwa Sonangol imebaini kuhamishwa kwa kiasi cha dola za Marekani milioni 67 kwenye akaunti ya Dubai.

Wachunguzi pia wataangalia malipo ya kila mwezi yaliyoanzishwa baada ya Isabel kuingia madarakani, ambapo kampuni moja ya Ureno ilikuwa inalipwa kiasi cha Euro milioni 10.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.