Pata taarifa kuu
DRC

Upinzani nchini DRC waitisha maandamano mengine kushinikiza rais Kabila kung'oka

Upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo umewataka kwa mara nyingine wafuasi wake kuandamana siku ya Jumanne kushinikiza kuondoka madarakani kwa rais Joseph Kabila licha ya mamlaka nchini humo kuzuia maandamano.

Wafuasi wa chama cha upinzani cha UDPS wakiwa nje ya makao makuu ya chama chao mjini Kinshasa.
Wafuasi wa chama cha upinzani cha UDPS wakiwa nje ya makao makuu ya chama chao mjini Kinshasa. Junior KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa chama kikuu cha upinzani UDPS Augustin Kabuya amesisitiza kuwa maandamano yao ya siku ya Jumanne yataendelea kama yalivyopangwa licha ya kuzuiwa na polisi.

Chama hicho kinasema kuwa maandamano ya siku ya Jumanne yanalenga kuongeza shinikizo kwa rais Kabila na kutaka pia uchaguzi mkuu ufanyike mwishoni mwa mwaka huu kama ilivyokubaliwa kwenye makubaliano ya Desemba 31 mwaka jana.

Kwa mujibu wa makubaliano haya yaliyosimamiwa na baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini DRC ambayo yaliwakutanisha upande wa Serikali na wapinzani, yalitamatika Desemba 31 mwaka jana walikubaliana uchaguzi mkuu ufanyike mwishoni mwa mwaka huu.

Baada ya shinikizo kutoka kwa jumuiya ya kimataifa tume ya uchaguzi nchini DRC CENI ilitangaza kalenda mpya ya tarehe ya kufanyika kwa uchaguzi mkuu mpya mwishoni mwa mwaka 2018 ili kupata mtu ambaye atarithi nafasi ya rais Joseph kabila aliyemaliza muhula wake mwezi Desemba mwaka jana.

Hata hivyo chama cha UDPS kinasema kuwa kwa upande wao hawatambui kalenda mpya iliyotangazw ana tume ya uchaguzi.

Upinzani nchini DRC unashinikiza kuondoka madarakani kw arais Kabila mwishoni mwa mwaka huu wakiamini kuwa uchaguzi unaweza kufanyika.

Tarehe 30 ya mwezi Novemba upinzani ulijaribu kuandaa maandamano dhidi ya utawala wa rais Kabila lakini hata hivyo mamlaka nchini DRC ziliyazuia na polisi walitumia nguvu kuwatawanya wafuasi wa upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.