Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/02 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 24/02 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

DRC: Mkuu wa tume ya kulinda amani akutana na rais Kabila

media Jean-Pierre Lacroix, mkuu wa tume za kulinda amani wa umoja wa Mataifa. 11 July 2017 UN Photo/Manuel Elias

Mkuu wa tume za kulinda amani wa umoja wa Mataifa mwishoni mwa juma amekutana na rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila na kusisitiza kuhusu umuhimu wa kuimarisha usalama na kufanyika kwa uchaguzi mkuu ulio huru na haki.

Mkutano kati ya Jean-Pierre Lacroix na rais Kabila umekuja ikiwa ni juma moja tu limepita toka kuuawa kwa wanajeshi 14 wa kulinda amani kutoka Tanzania ambao walishambuliwa na waasi wa ADF jimboni Kivu Kaskazini.

Lacroix Ijumaa ya wiki iliyopita aliwatembelea zaidi ya askari 30 waliojeruhiwa katika shambulio la Desemba 7.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka MONUSCO zinasema kuwa Lacroix na rais Kabila walizungumzia kuhusu shambulio dhidi ya walinda amani, likiwa ni shambulio baa zaidi katika historia ya umoja wa Mataifa kwa walinda amani wake kuuawa kwa idadi kubwa.

Chanzo hicho cha MONUSCO kimeongeza kuwa pia walizungumzia kuhusu hali ya usalama kwenye maeneo mengine ya nchi pamoja na mzozo wa kisiasa nchini DRC.

Lacroix alimueleza rais Kabila kuwa "suala la usalama mashariki mwa DRC ni suala la kuunganisha nguvu za pamoja".

"Ushirikiano na nchi nyingine za jirani ni muhimu sana katika kudhibiti usalama," alinukuliwa Lacroix wakati alipokuwa akizungumza na kituo cha Redio cha umoja wa Mataifa.

Eneo la mashariki mwa DRC kwa miongo kadhaa limekuwa likishuhudia makabiliano kati ya makundi ya waasi na vikosi vya Serikali ambapo kwa mwaka huu mashambulizi yameongezeka zaidi.

Jimbo la Kivu kaskazini linapaka na nchi za Uganda na Rwanda na makundi kutoka pande hizo mbili yamekuwa yakitekeleza utekaji nyara na mauaji mashariki mwa DRC.

Nchi ya DRC pia imejikuta ikitumbukia kwenye mzozo wa kisiasa baada ya rais Kabila kukataa kuondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wake mwezi Desemba mwaka jana na kuahirisha zoezi la kura hadi Desemba mwaka 2018.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana