Pata taarifa kuu
DRC-UBAKAJI-HAKI

Mbunge wa mkoa wa Kivu Kusini ahukumiwa kifungo cha maisha jela

Mahakama ya kijeshi katika jimbo la Jimbo la Kivu Kusini nchini DRC imehukumu maisha jela mbunge Fréderic Batumike na watu wengine 11 kwa kosa la kuwabaka watoto Mashariki mwa nchi hiyo, ikiwa ni pamoja na mtoto wa mwaka mmoja.

Wanamgambo 11 ikiwa ni pamoja na mbunge Frederic Batumike wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuwabaka wasichana zaidi ya 46 katika kijiji cha Kavumu, mashariki mwa DRC.
Wanamgambo 11 ikiwa ni pamoja na mbunge Frederic Batumike wamehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kuwabaka wasichana zaidi ya 46 katika kijiji cha Kavumu, mashariki mwa DRC. RFI
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa pia wametakia kulipa fidia kwa wahanga ya dola za marekani kati ya 5000 na 15.000.

Hukumu ime tolewa jana huko Kavumu katika jimbo la kivu ya kusini.

Awali mbunge wa jimbo la mkoa huo Frederick Batumike alikuwa aliomba kuongezwa majaji wengine wawili, ombi ambalo lilitupiliwa mbali, na mahakama kuomba kesi hiyo iendelee kusikilizwa.

Hukumu ya mahakama ya kijeshi dhidi ya watuhumiwa hao imekaribishwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanaharakati wa haki za binadamu wanauona kwamba kesi hiyo ni muhimu sana na ina uzito mkubwa katika harakati za kukabiliana na hali ya kutowaadhibu wa husika wa matukio mbalimbali ya ubakaji na mauaji ama impunity ambapo wasichana zaidi ya 40 wamebakwa.

Msemaji wa muungano wa mawakili wa upande wa utetezi Wakili Charles Kubaka Sikura amesema licha ya kesi hiyo kuanza kwa kuchelewa, wameridhishwa na hatua hiyo.

Wakati huo huo wmawakili wa mbunge Fréderic Batumike amekosoa namna kesi hiyo ilivyoendeshwa, wakisema majaji wamekua wakishinikizwa na baadhi ya vigogo serikalini kuchukua hatua kali dhidi ya mteja wao. Hata hivyo wamesem awatakata rufaa.

Kwa upande wa raia wameomba mali ya mbunge huyo ipewe waathirika wa kitendo hicho cha ubakaji ili waweze kujimudu kimaisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.