Pata taarifa kuu
URUSI-CAR-UNSC-USALAMA

Urusi yataka kuipa silaha Jamhuri ya Afrika ya Kati

Urusi imeomba Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuiondolea Jamhuri ya Afrika ya Kati vikwazo vyasilaha ili kuvipa silaha za kutosha vitengo viwili vya jeshi vinavyoandaliwa kwa kudumisha ulinzi katika nchi hiyo ambayo usalama unaendelea kudorora kila kukicha.

Askari wa kikosi cha Minusca kutoka Senegalwakipiga doria katika mitaa ya Bangui mnamo tarehe 10 Desemba 2015, siku mbili baada ya mapigano mapya kuzuka.
Askari wa kikosi cha Minusca kutoka Senegalwakipiga doria katika mitaa ya Bangui mnamo tarehe 10 Desemba 2015, siku mbili baada ya mapigano mapya kuzuka. MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ombi hili linaonekana liko sambamba na matakwa ya Umoja wa Mataifa ya kuimarisha jeshi dhaifu la nchi hiyo. Hata hivyo, Ufaransa una wasiwasi kuhusu uhifadhi wa silaha na risasi zitakozotolewa, kwa mujibu wa vyanzo kutoka baraza la Usalam la Umoja wa Mataifa.

Uamuzi wa kukubali ombi la Urusi uliwekwa chini ya "utaratibu wa kusalia kimya" mpaka leo Jumatano saa 02:00 usiku saa za kimataifa, kwa mujibu wa wanadiplomasia. Ombi hilo litachukuliwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuwa limepitishwa ikiwa hakutapatikana mwanachama ambaye atavunja ukimya huo.

Silaha za kwanza zinaweza kuwasili nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati siku ya Jumatatu Desemba 18, na zingine mnano Februari 1 na Aprili 1, kwa mujibu wa Moscow. Bataliani mbili zinazojumuisha askari 1,300 zitapewa silaha hizo, ikiwa ni pamoja bastola 900 aina ya Makarov, bunduki 5200 aina ya AKM silaha za kivita 140, silaha zingine za kivita 840 aina ya Kalashnikov,...

Urusi pia imependekeza kutoa mafunzo kwa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati kwa matumizi ya silaha hizo, hoja ambayo itapasishwa na Umoja wa Mataifa.

Kwa mujibu wa chanzo cha kidiplomasia, Ufaransa hivi karibuni ilivunja utaratibu wa ukimya wa kwanza kwa kuiomba Urusi kutoa maelezo zaidi. Kwa upande wa Ufaransa, inatarajiwa kwamba vikwazo vya silaha vilivowekwa dhidi ya Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo mwaka 2013, vinaweza kufutwa, iikiwa mchakato huu kwa utasimamiwa na kufuatiliwa kwa karibu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.