Pata taarifa kuu
LIBERIA-UCHAGUZI-SIASA

Duru ya pili ya uchaguzi kufanyika Desemba 26 nchini Liberia

Tume ya Uchaguzi nchini Liberia (NEC) imetangaza kwamba duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo itafanyika Desemba 26 kati nyota wa zamani wa mpira wa miguu George Weah na Makamu wa Rais, Joseph Boakai, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jerome Korkoya, ametangaza.

George Weah,mgombea wa chama cha CDC akipiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura vya Monrovia, Liberia, Oktoba 10, 2017.
George Weah,mgombea wa chama cha CDC akipiga kura katika moja ya vituo vya kupigia kura vya Monrovia, Liberia, Oktoba 10, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

"Kulingana na maagizo ya Mahakama Kuu kwa Tume ya Uchaguzi (...) duru ya pili ya uchaguzi wa urais 2017 itafanyika Jumanne, Desemba 26," Bw Korkoya alisema katika mkutano na waandishi wa habari, huku akiongeza kuwa kampeni ya uchaguzi tayari imefunguliwa hadi Desemba 24 saa 05:59 usiku.

Duru ya pili, ambayo awali iliyopangwa kufanyika Novemba 7, iliahirishwa na Mahakama Kuu, ambayo iliamuru NEC kuchunguza madai ya mgombea, ambaye alichukua nafasi ya tatu katika duru ya kwanza Oktoba 10, akipata 9.6% ya kura, Charles Brumskine, ambaye Bw Boakai alijiunga naye.

Lakini Mahakama ilifutilia mbali madai hayo, kwa kura nne dhidi ya moja, na hivyo kuruhusu duru ya pili ya uchaguzi kufanyika, kwa masharti kwamba NEC irejelee upya orodha za uchaguzi, zilizokosolewa, kwa mujibu wa VOA Afrique.

"Tunafahamu kwamba siku hii ni baada ya Krismasi, na tunatoa wito kwa wapiga kura wote waliosajiliwa kuchangia ili kufanikisha hili, kwa mapenzi ya demokrasia yetu," Bw Korkoya aliongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.