Kusikiliza Pakua Podcast
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
  Uchambuzi na makala 23/09 04h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
  Uchambuzi na makala 23/09 05h30 GMT
 • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
  Uchambuzi na makala 22/09 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
 • Kampuni kubwa ya kitalii duniani Thomas Cook yafilisika
 • Kanisa Katoliki nchini Burundi laishtumu serikali ya Burundi
 • Chanjo ya pili ya Ebola kuanza kutolewa nchini DRC mwezi Oktoba
Afrika

Umoja wa Ulaya watishia kusitisha misaada yake DRC

media Serikali ya DRC imepiga marufu maandamano na mikusanyiko. REUTERS/Kenny Katombe/File Photo

Umoja wa Ulaya umeionya serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya congo kuwa utasitisha misaada yake kusaidia nchi hiyo kufanikisha Uchaguzi Mkuu mwaka ujao, iwapo itaendelea kutumia maafisa wa usalama kuwanyanyansa wanasiasa wa upinzani na mashirika ya kiraia.

Katika ripoti yake Umoja wa Ulaya umesema serikali ya Kinshasa imeendelea kuwakamata, kuwazuia wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao pamoja na wanaharakati wa haki za binadamu kwa sababu ya harakati zao za kuikosoa serikali ya rais Joseph Kabila.

Upinzani umefurahishwa na ripoti hiyo. Akihojiwa na RFI, Gregoire Kiro, mbunge wa chama cha upinzani cha RCD-Kml akiwa Kinshasa amesma hatua hiyo itapelekea visa vya unyanyasaji vinavyoendelea kusitishwa mara moja.

Upande wa serikali, wao wanaona kuwa Umoja wa Ulaya hauna sababu ya kutoa mashinikizo yoyote wakati mchakato wa uchaguzi unaendelea vizuri.

Mbali na Umoja wa Ulaya, Ubelgiji ambao ni wakoloni wa zamani wa DRC, wamesema wametenga Euro milioni 5.8 kuisaidia Tume ya Uchaguzi kufanyika hilo.

Tume ya Uchaguzi nchini DRC CENI tayari imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu utafanyika mwezi Desemba mwaka ujao.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana