Pata taarifa kuu
DRC-UBAKAJI-HAKI

Kesi ya ubakaji kusikilizwa Kavumu, mashariki mwa DRC

Kesi ya ubakaji ya Kavumu, mashariki mwa DR Congo imeanza tena kusikilizwa, ambapo mtuhumiwa mkuu ambae ni mbunge wa jimbo la mkoa huo Frederick Batumike alikuwa ameomba kuongezwa majaji wengine wawili, ombi ambalo limetupiliwa mbali, na mahakama kuomba kesi hiyo iendelee kusikilizwa.

Watuhumiwa kumi na wanane wanaaminika kuwa wamehusika na utekaji nyara na ubakaji wa usiku wa wasichana katika kijiji cha Kavumu, karibu na mji wa Bukavu watasikilizwa.
Watuhumiwa kumi na wanane wanaaminika kuwa wamehusika na utekaji nyara na ubakaji wa usiku wa wasichana katika kijiji cha Kavumu, karibu na mji wa Bukavu watasikilizwa. Google Maps
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati watetezi wa haki za binadamu wamepongeza hatua hiyo na kuona kwamba kesi hiyo ni muhimu sana na ina uzito mkubwa katika harakati za kukabiliana na hali ya kutowaadhibu wa husika wa matukio mbalimbali ya ubakaji na mauaji ama "impunity" ambapo wasichana zaidi ya 40 wamebakwa huku mwanaharakati wa haki za binadamu akiuawa na waasi ambao wamekuwa wakilindwa.

Msemaji wa muungano wa mawakili wa upande wa utetezi Wakili Charles Kubaka Sikura amesema licha ya kesi hiyo kuanza kwa kuchelewa, wameridhishwa na hatua hiyo.

Hayo yakijiri shirika linalo tetea haki za waandishi wa habari nchini humo JED limelaani shambulio dhidi ya kituo cha radio na televisheni Kindu Maniema RTKM Mashariki mwa Congo na kumtuhumu waziri wa mambo ya ndani Emmanuel Ramadhani Shadari ambae upande wake ametupilia mbali tuhuma dhidi yake.

JED linasema, tukio hilo linadaiwa kutekelezwa na kundi la askari polisi walioshambulia na kundoka na vifaa vya radio hiyo na kuwatia nguvuni watu wote waliokuwepo kituoni hapo wakiwemo pia waandishi wa habari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.